Amri ya utekelezaji vikwazo dhidi ya Russia nambari 13660 ilitiwa saini kwa mara ya kwanza na Marekani mnamo Machi 6, 2014.
Katika hati hiyo, Barack Obama Rais wa wakati huo wa Marekani aliwawekea vikwazo shakhsia binafsi na taasisi zilizodaiwa kuhusika na kukiukwa mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Ukraine.
Vipengee vya dikrii hii ya kiutendaji pia vinahusu vikwazo vya safari kwa watu mahsusi waliotajwa na wale waliohusika na kuunganishwa kisiwa cha Crimea na Russia.
Marekani imerefusha muda wa vikwazo dhidi ya Russsia kwa mwaka mwingine mmoja katika hali ambayo nchi hiyo na Marekani zilikuwa tayari zimeanza mchakato wa mazungumzo kati yao kwa ajili ya kutatua masuala ya pande mbili na mzozo wa Ukraine.
Duru ya karibuni ya mazungumzo ya wawakilishi wa Russia na Marekani ilimalizika jana alasiri mjini Istanbul Uturuki baada ya masaa sita ya mazungumzo kuhusu kuhuisha mchakato wa shughuli za balozi za nchi mbili hizo.
Mazungumzo ya jana ya Istanbul kati ya Moscow na Washington yamefanyika baada ya Marekani na Russia kutathmini vyema mijadala iliyofanywa na wajumbe wao wa ngazi ya juu wakiongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, tarehe 18 Februari.
342/
