Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na Taasisi ya Gallup yanaonyesha kuwa, uungaji mkono wa umma wa Marekani kwa Israel umefikia kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Kulingana na gazeti laYediot Aharonot, uungaji mkono wa watu wa Marekani kwa Israel umefikia kiwango cha chini kabisa tangu 2000 na umepungua hadi 54%.
Uchunguzi huo mpya wa maoni ya Taasisi ya Gallup, ambayo kila mwaka huchunguza mtazamo wa watu wa Marekani kwa nchi mbalimbali duniani, unaonyesha kupungua kwa uungwaji mkono wa watu wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kuwa: Baada ya vita vya Gaza, ni thuluthi moja tu ya Wademokrat walio na mtazamo chanya dhidi ya Israel, huku idadi hii kwa Warepublican wa Marekani inakadiriwa kuwa asilimia 83.
Matokeo hhayo yanaonyesha kuwepo kwa pengo la asilimia 50 kati ya Wademokrat na Warepublican wanaoiunga mkono Israel, jambo ambalo linaashiria kutokuwa tayari kwa wafuasi wa chama cha Democratic kuunga mkono misimamo ya utawala wa Kizayuni.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kukabiliwa na mashinikizo makubwa na kutolewa miito ya kutengwa hata katika uga wa michezo kutokana na kutenda jinai za kutisha katika Ukanda wa Gaza dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
342/
