4 Machi 2025 - 23:27
Source: Parstoday
Qatar: Kutumia chakula kama silaha ya vita ni kukiuka sheria za kimataifa

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imetoa taarifa na kutangaza kuwa, inapinga vikali suala la raia kufa njaa na kutumiwa chakula kama silaha ya vita katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, tunakaribisha kwa mikono miwili hatua yoyote ya jamii ya kimataifa ya kuishinikiza na kuilazimisha Israel kuhakikisha usalama na kuendelea kuwasili kwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wote wa Gaza.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Qatar imebainisha kuwa, tunalaani vikali uamuzi wa utawala wa "Israel" wa kusitisha misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Kusimamisha  misaada ya kibinadamu huko Gaza ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano, sheria za kimataifa za kibinadamu, Mkataba wa Geneva na mafundisho ya dini.

Hatua ya Israel ya kuzuia kuingizwa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imelaaniwa na Misri na Saudi Arabia, huku nchi mbili hizo zikisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.

Kabla ya hapo, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina ililaani pia uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza na kuonya juu ya madhara ya hatari ya hatua hiyo katika mgogoro wa sasa hususan katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha