Kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni na kushambuliwa kwa mabomu na makombora Wapalestina wa Ghaza, mbali na kuuawa shahidi na kujeruhiwa raia wapatao 700 wakiwemo watoto, maafisa watano waandamizi wa Hamas pia ni miongoni wa waliouawa shahidi akiwemo Essam Al-Dalalis, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina.
Afisa mwingine wa Hamas aliyeuawa shahidi ni Behjat Abu Sultan, ambaye ni mmoja wa viongozi mashuhuri wa Hamas anayehusika na operesheni za ndani huko Ghaza. Abu Sultani aliwahi kushika nyadhifa kadhaa muhimu katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Idara za Intelijensia za serikali ya Hamas huko Ghaza.
Ahmed Omar Al Khati, maarufu kwa lakabu ya Abu Omar, ni Shahidi wa tatu wa jinai ya Jumanne asubuhi iliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza. Yeye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Sheria ya serikali ya Hamas katika Ukanda wa Ghaza na anajulikana ka mchango mkubwa aliotoa katika kuimarisha mfumo wa sheria za Kiislamu huko Ghaza, ambapo mwaka 2021 alichaguliwa kuwa mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Polisi cha Rabat.
Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Israel la Yediot Aharonot, afisa wa nne wa ngazi ya juu wa Hamas aliyeuawa shahidi katika jinai ya jana asubuhi ni Jenerali Mahmoud Abu Watfa, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Hamas huko Ghaza. Kwa mujibu wa gazeti hio Abu Watfa aliuawa shahidi pamoja na familia yake katika shambulio la anga lililolenga nyumba yake huko katika mji wa Ghaza. Baada ya kuanza kutekelezwa usitishaji vita, katika mazungumzo na mkazi mmoj wa Ghaza, Abu Atfa alisisitizia dhamira ya Hamas ya kuujenga upya Ukanda wa Ghaza na akasema: "Tutaijenga upya Ghaza na kuifanya imara zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma".
Abu Obeidah al-Jamasi ni mwanachama mwingine mwandamizi wa Hamas aliyeuwa shahidi katika jinai ya utawala wa Kizayuni. Yeye aliwahi kuwa mkuu wa idara ya uongozi kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
Kwa mujibu wa habari za duru za Palestina, kuuawa shahidi maafisa hao waandamizi watano wa Hamas kumethibitishwa.../
342/
Your Comment