Taarifa hiyo inasema: "Viongozi wa ugaidi wa kiserikali wa Marekani na Ulaya, pamoja na waungaji mkono wa utawala katili wa Kizayuni, wamefanya njama nyingine na kuliita Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu—nguvu kubwa zaidi ya kupambana na ugaidi duniani—kuwa ni magaidi! Bila shaka, uadui wa upande huu muovu ni heshima kubwa kwa IRGC."
Wizara imesisitiza kuwa hatua hii, iliyochukuliwa kwa utii usio na masharti kwa Marekani na utawala wa Kizayuni, haitadhuru azma ya taasisi hii tukufu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa Ulaya ni kimbilio la magaidi na kusisitiza kuwa Wizara ya Usalama itabaki kuwa mshirika wa bega kwa bega na IRGC katika kulinda nchi dhidi ya fitna zote.
Your Comment