Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) – ABNA – baada ya kumteka nyara kwa haraka Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika baadhi ya duru za kisiasa za Washington - hasa miongoni mwa Republican - imejengeka dhana kwamba inawezekana kurudia ule ule mfano nchini Iran.
Lakini jarida la Newsweek katika makala yake ya uchambuzi iliyoandikwa na Bodi yake ya Uhariri limeonya kuwa ulinganisho huu ni wa kupotosha na hatari, na limeasisitiza kuwa Iran kwa mtazamo wa muundo wake wa kisiasa na kijeshi na kiwango cha utayari wake wa migogoro, ina tofauti za kimsingi na Venezuela.
Licha ya kwamba "Donald Trump" Rais wa Marekani Jumatatu alisema kwamba Jenerali "Dan Caine" Mwenyekiti wa Wakuu wa Wafanyakazi Pamoja wa Marekani alimjulisha kwamba mgogoro wowote na Iran utaweza kukomeshwa kwa urahisi, lakini jenerali huyo alionya kuwa uhaba wa risasi na kutokuwepo kwa msaada wa washirika, kunaifanya operesheni kama hiyo kuwa na hatari kubwa zaidi kuliko operesheni ya Venezuela.
Marekani alfajiri ya Jumamosi tarehe 3 Januari iliyopita ilishambulia malengo nchini Venezuela na kumkamata Maduro; yeye sasa anashtakiwa New York kwa mashtaka ikiwa ni pamoja na ugaidi unaohusiana na dawa za kulevya kulingana na uainishaji wa Marekani.
Wakati Trump anachunguza mipango ya kupindua serikali ya Iran, hali za ndani za Iran zinafanya kurudia kile Newsweek anachokiita "wakati wa Maduro", kuwa ngumu zaidi kuliko Caracas. Jarida hili limetoa sababu tano za tathmini hii:
1. Ayatollah Khamenei si lengo rahisi
Tofauti na Maduro, Ayatollah Khamenei kiongozi wa Iran si mtu ambaye anaweza kuzingirwa au kukamatwa kwa urahisi. Yeye yuko chini ya ulinzi wa kitengo cha wasomi cha usalama cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi na analindwa ndani ya mfumo wa ulinzi. Maafisa wa zamani wa Marekani wanaamini kwamba jaribio lolote la dhati la kumkamata Ayatollah Khamenei linaweza kusababisha si kuvunjika kwa kisiasa, bali kuongezeka kwa mvutano kwa kiwango kikubwa.
2. Muundo wa serikali ya Iran hautaanguka kwa kuondolewa kwa kiongozi
Kwa mujibu wa uchambuzi huu, mfumo wa kisiasa wa Iran una mshikamano zaidi ikilinganishwa na muundo uliokuwepo karibu na Maduro. Taasisi za kisiasa, kijeshi na kidini nchini Iran zimeunganishwa kwa kina na zimejiandaa kwa matukio ya mauaji au kukosekana kwa uongozi.
Newsweek akimnukuu New York Times aliandika kwamba Ayatollah Khamenei amewateua waandamizi wa ngazi nne kwa kila wadhifa nyeti na amezuia duru za maamuzi ili hata katika tukio la kukatika kwa mawasiliano au kuuwawa kwa makamanda wakuu, mwendelezo wa utawala uhifadhiwe.
3. Iran iko tayari kwa vita
Tofauti na Venezuela, Iran kwa miezi kadhaa imekuwa ikijiandaa kwa uwezekano wa mapigano ya moja kwa moja ya kijeshi. Vikosi vyake viko katika hali ya juu zaidi ya kusubiri, na mifumo ya makombora imepangwa upya katika mipaka ya magharibi na pwani ya Ghuba ya Uajemi.
Ali Larijani, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran amesema: "Tumezipitia na kuziondoa udhaifu wetu. Ikiwa tutalazimishwa kuingia vitani, tutajibu." Picha za satelaiti zilizochapishwa na shirika la habari la Reuters pia zinaonyesha shughuli kubwa za uimarishaji na ujenzi upya katika vituo vya nyuklia na makombora vya Iran.
4. Vita havitabaki ndani ya mipaka ya Iran
Newsweek anaonya kwamba mapigano yoyote na Iran hayatabaki ndani ya ardhi ya nchi hii. Tehran ina mtandao wa washirika na makundi yenye silaha nchini Lebanon, Iraq na Yemen, ambayo yanaweza kusababisha kufunguliwa kwa nyanda nyingi dhidi ya maslahi ya Marekani na Israeli.
Wachambuzi wanaogopa kwamba kuporomoka kwa ghafla nchini Iran kunaweza kusababisha ombwe la nguvu ambalo litatishia utulivu wa Mashariki ya Kati yote.
5. Changamoto ngumu za kijiografia na vifaa
Hatimaye, eneo la kijiografia la Iran, umbali wake mkubwa na ukosefu wa msaada wa washirika, hufanya shambulio lolote kuwa gumu zaidi kuliko operesheni ya Venezuela.
Kwa maoni ya Newsweek, Iran iko ndani kabisa ya Mashariki ya Kati, na jambo hili linahitaji vikosi vya Marekani kufanya operesheni kutoka vituo vyao huko Ulaya au Ghuba ya Uajemi chini ya amri ya CENTCOM. Pia upinzani wa Uingereza kutumia vituo vyake vya kimkakati kwa shambulio bila kinga ya kisheria iliyo wazi, umeongeza utata wa hali hiyo.
Kwa muhtasari, Newsweek anaamini kuwa uzoefu wa Venezuela unaweza kuwajaribu watoa maamuzi Washington, lakini si kielelezo kinachofaa kwa Iran. Utawala wa Iran una mizizi zaidi na uko tayari zaidi, na jaribio lolote la kuubadilisha kwa nguvu linaweza kusababisha vita vya kikanda na mshtuko katika masoko ya nishati ya dunia; gharama ambayo itakuwa mbali zaidi ya mipaka ya Iran.
Your Comment