26 Februari 2026 - 09:30
Source: ABNA
Kamati ya Uratibu wa Makundi ya Muqawama ya Iraq: Wakaaji wa Kiamerika wanapaswa kuondoka

"Wakaaji wanaendelea kukiuka anga ya Iraq; iwe kwa njia ya ndege zisizo na rubani au kwa ndege zao za kivita. Hatua hizi ni tishio kubwa kwa usalama, utulivu na uadilifu wa nchi na ni uvamizi wa wazi juu ya mamlaka na hadhi ya serikali ya Iraq."

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) – ABNA – Kamati ya Uratibu wa Makundi ya Muqawama ya Iraq katika msimamo wake ilitangaza: Asili ya uhusiano kati ya Iraq na Marekani haikujengwa kwa msingi wa usawa kati ya nchi mbili huru; kwa sababu Washington bado inaingilia mambo ya ndani ya Iraq na hata huamua ni watu gani wa kisiasa wanaruhusiwa kushikilia nyadhifa za serikali na ni nani watengwe; hivyo kwa msingi wa kigezo cha mapenzi ya Amerika na ndani ya mfumo wa mkabala unaofuatwa katika sera zake za kutawala.

Kamati hii imeongeza: Bila shaka wakaaji wanaendelea kukiuka anga ya Iraq; iwe kwa njia ya ndege zisizo na rubani au kwa ndege zao za kivita. Hatua hizi ni tishio kubwa kwa usalama, utulivu na uadilifu wa nchi na ni uvamizi wa wazi juu ya mamlaka na hadhi ya serikali ya Iraq.

Kamati ya Uratibu imebainisha: Sisi katika Muqawama wa Iraq tunasisitiza kwamba Marekani haijashikilia ahadi zake zote na hatujashuhudia hatua yoyote ya kweli ya kutekeleza sehemu zilizobaki za makubaliano na serikali ya Iraq ambayo yanabainisha kuondoka kabisa kwa vikosi vyote vya kigeni kutoka ardhi na anga ya Iraq. Kukawia huku kwa kukwepa na kukwama kutekeleza ahadi, kunatulazimu kuchukua majukumu yetu ya kidini na kimaadili katika kuchukua misimamo inayostahili taifa letu na haki yake halali ya kumaliza ukaliaji; endapo watasisitiza kuendelea kukaa na kulazimisha mapenzi yao kwa nchi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha