Idara hiyo ya Upepelezi ya Israel DEBKA imezinukuu duru za Marekani na kuripoti kuwa ndege za Marekani zisizo na rubani zilikuwa zikiichunguza nyumba moja huko katika mji wa Sirte alikozaliwa Gaddafi huku nyumba hiyo ikizingirwa pia na wanajeshi wa Marekani na Uingereza.
Idara ya Upelelezi ya Israel DEBKA imesisitiza kuwa wanajeshi wote wa Marekani na Uingereza walikuweko katika eneo hilo huko Sirte hatua ambayo inakinzana na mamlaka na agizo la Umoja wa Mataifa lililopiga marufuku kupaa ndege katika anga ya Libya.
Debka imeongeza kuwa ripoti mbalimbali kuhusiana na siku za mwisho za Gaddafi zinaonyesha kuwa, kiongozi huyo wa zamani wa Libya alipuuza tahadhari zilizokuwa zikimlinda kwa miaka kadhaa na kwamba Gaddafi hakuhofia kutumia satalaiti na simu za mkononi ambazo zilipelekea kunaswa mahali alipo.
Muammar Gaddafi alitiwa nguvuni na kuuawa na vikosi vya wanamapinduzi wa Libya Alkhamisi iliyopita baada ya ndege za Nato kuulenga msafara wake huko magharibi mwa mji wa Sirte.
19 Machi 2011 - 20:30
News ID: 274395
Idara ya Upelelezi ya Israel imesema kuwa wanajeshi wa Marekani na Uingereza waliyazingira maficho ya Muammar Gaddafi wiki mbili kabla ya kukamatwa na kuuawa.