Mtandao wa satelaiti wa Al-Aqsa umetangaza: Matangazo ya Idhaa ya Al-Aqsa yamesimamishwa katika Satelaiti zote za Kimataifa. Na Shirika lolote la Satelaiti litakaloendelea na urushaji wa matangazo na habari za Idhaa ya Al-Aqsa litakumbana na vikwazo vikubwa vya kiuchumi.

15 Machi 2025 - 18:15

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna - : Harakati ya Hamas imelaani vikali uamuzi wa pamoja wa Marekani na Ulaya wa kuondoa mtandao wa Satelaiti wa Idhaa ya Al-Aqsa katika Satelaiti zote za Kimataifa na kuuona uamuzi huo kuwa ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa vyombo vya habari na haki halali ya Taifa la Palestina ya kufikisha sauti yake kwa walimwengu.

Mtandao wa Satelaiti wa Al-Aqsa umebainisha kuwa: Matangazo ya Idhaa ya Al-Aqsa yamesimamishwa katika Satelaiti zote za Kimataifa. Na Shirika lolote la Satelaiti litakaloendelea na urushaji wa matangazo na habari za Idhaa ya Al-Aqsa litakumbana na vikwazo vikubwa vya kiuchumi.

Habari Pichani | Hamas: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina

Radiamali ya Hamas juu ya hatua ya Marekani na Ulaya katika kusimamisha (kuzuia) urushaji wa matangazo ya Idhaa ya Al-Aqsa. Hamas imesema: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina.

Habari Pichani | Hamas: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina

Hamas imefahamisha kuwa hatua hiyo inaendana na majaribio yaliyofeli ya adui ya kukandamiza uhuru wa kujieleza na kufunga nafasi kwenye majukwaa yote, jambo ambalo linafichua ugaidi uliopangwa dhidi ya ardhi na hifadhi za Palestina.

Habari Pichani | Hamas: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina

Harakati hii ya Hamas imesisitiza kuwa: Juhudi zote za uvamizi zinazolenga kuminya, kukandamiza sauti ya wapalestina na kupindisha ukweli na uhakika, zitafeli. Sauti ya Upinzani (Muqawamah) vile vile itaendelea kuwa hai na kusikika, na kuwakilisha haki halali za Palestina hadi uhuru (wa Palestina) utakaporudi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha