Tukio hili ni ushahidi wa kuendelea kwa mapenzi ya kweli kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kwamba ujumbe wake bado unaishi katika nyoyo za wafuasi wake.

23 Agosti 2025 - 02:05

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii, (Ijumaa: 22-08-2025) yamefanyika Masira makubwa Kigogo Post, Dar-es-salaam - Tanzania katika kuhuisha kumbukumbu ya Kifo cha Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) yaliyoanzia maeneo ya Ilala Boma hadi Masjid Al-Ghadir (Kigogo Post).

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

Tukio hili lina umuhimu mkubwa kwa Waislamu, hususan wafuasi wa Mtume (s.a.w.w) na kizazi chake kitukufu, kwani linawakilisha hali ya mapenzi, utiifu, na heshima ya dhati kwa Mtume wa mwisho aliyeleta mwanga wa Uislamu kwa wanadamu wote.

Mambo Muhimu Yaliyokusudiwa Katika Masira Haya:
1. Kuhuisha Historia na Maisha ya Mtume (s.a.w.w):

Ni fursa kwa Waislamu wa Tanzania na Dunia kwa ujumla, kukumbuka maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) - yaliyojaa mafunzo mbalimbali. Sehemu ya mafunzo hayo ni ile hali ya juu wa maadili, ya Mtume Muhammad(s.a.w.w), huruma yake kwa waja wa Mwenyezi Mungu, subira yake, na uadilifu wake. Tukio hili la kuhuisha kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) linawahamasisha watu kumfuata Mtume (s.a.w.w) katika maisha ya kila siku.

2. Maombolezo na Mashairi ya Marsiya:

Kupitia mashairi, hotuba na maombolezo, masira haya yanakuwa jukwaa la kiroho la kuhuisha maumivu ya kuondoka kwa kipenzi cha Umma(s.a.w.w), na kwa wakati huo kuimarisha imani na mshikamano wa kijamii.

3. Elimu na Ustawi wa Kijamii:

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

Masira haya si ya huzuni tu, bali pia ni njia ya kuelimisha jamii kuhusu nafasi ya Qur’an na Ahlul-Bayt (as) kama vyanzo vya uongofu - kama alivyousia Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) katika Hadithi ya Thaqalayn:

“Nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur’an) na Kizazi changu - Ahlul-Bayt wangu; mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu.”

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

4. Umoja wa Kiislamu:

Katika nyakati za migawanyiko, kumbukumbu hizi za kuhuisha Kifo cha Mtume wa Umma, Muhammad (s.a.w.w) huleta Waislamu pamoja, huku zikisisitiza ushirikiano, umoja baina yao, huruma na mshikamano wa kimapokeo wa Dini Tukufu ya Kiislamu.

Tukio hili ni ushahidi wa kuendelea kwa mapenzi ya kweli kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kwamba ujumbe wake bado unaishi katika nyoyo za wafuasi wake.

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

Masira Kubwa Ya Kumuomboleza Mtume Muhammad(s.a.w.w) Yafanyika Dar-es-Salaam – Waislamu Waihuisha Kumbukumbu ya Kifo Chake kwa Mapenzi na Umoja +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha