Baadhi ya Mabedui walikuwa wakimfanyia Mtume (s.a.w.a) madai ya fadhila kwa kusilimu kwao, kama Qur’ani inavyosema:
“Wanakuonea fadhila kwa kusilimu kwao.”
Basi Qur’ani ikawafunza adabu kwa kusema:
“Sema: Msinionee fadhila kwa Uislamu wenu; bali Allah ndiye anayekuoneeni fadhila kwa kuwaongoza kwenye imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.” (Al-Hujurāt: 17).
Msemo huu: "Elimika Usiwe Msomi" ni wito wa kuhusisha Elimu na Maadili. Elimu ya Kweli huonekana katika namna unavyowatendea wengine. Namna unavyofikiri kuhusu Haki na Uadilifu kwa kila Mwanadamu bila kujali Imani yake ya Kidini.