Kiongozi Muadham wa Mapinduzi ameeleza katika Mkutano na wahusika wa Hajj na baadhi ya Waumini waliotembelea Nyumba Tukufu (Al-Kaaba) kwamba: "Muundo na sura ya nje ya ibada hii ni ya kisiasa kabisa, lakini maudhui ya vipengele vyake ni ya kiroho na ya ibada, ili manufaa ya Wanadamu wote yaweze kutimizwa. Na leo, faida kubwa kwa Umma wa Kiislamu ni 'Umoja na Ushirikiano' ili kutatua matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu. Ikiwa umoja huu ungelikuwepo, matatizo kama ya Gaza na Yemen yasingekuwepo."
Imam Ali (a.s), Maisha yake yote yalikuwa ni Maisha ya kuweka uthabiti na kuimarisha nguzo na misingi ya Uislamu, pia kujitolea muhanga kwa kitu ghali na chenye thamani kubwa, ili kuhakikisha neno la Mwenyezi Mungu linakuwa juu, na neno la makafiri linakuwa chini.