Katika hafla iliyofanyika asubuhi ya jana katika Hoteli ya Central Yangon, Myanmar, Taasisi ya Kiislamu ya Al-Azhar ya nchi hiyo ilitoa shukrani zake kwa wanachama wa jamii ya Shia kutokana na mchango wao katika kuimarisha mshikamano wa amani na maelewano kati ya Waislamu, pamoja na kukuza urafiki kati ya dini na tamaduni tofauti. Hujjatul-Islam Haji Masoom Ali alikabidhiwa Tuzo Maalumu ya Taasisi hiyo kwa niaba ya jamii ya Shia ya jiji la Yangon.
Kimya cha jumuiya ya kimataifa kuhusu uonevu na uchokozi huu na kukosekana kauli za kuuzuwia, kinachukuliwa kuwa ni ushiriki katika jinai hizo, na matokeo yake pekee yatakuwa ni tishio kwa usalama wa dunia nzima. Vita havizai amani."