Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran, Ali Akbar Velayati, amesema watoto ni mstari mwekundu wa pamoja kwa ubinadamu, akisisitiza kuwa kuuawa kwa mtoto mmoja popote duniani ni sawa na kuua watoto wote wa wanadamu.
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameandika akirejea kusitishwa kwa mapigano huko Ghaza kwamba:
“Kuanza kwa kusitishwa mapigano huko Ghaza kunaweza kuwa nyuma ya pazia la kumalizika kwa kusitishwa mapigano mahali pengine.”