Hijja hii ilihudhuruwa na maswahaba wengi sana, inasemekana kuwa idadi yao ilikuwa takriban watu laki moja na ishirini na nne elifu (124000), watu hawa katika siku ya jummamosi tarehe 24 mwezi wa Dhilqa’adah wakiwa sanjari na mtume Muhammad s.a.w waliongozana kuelekea katika mji mtukufu wa Makka kwa ajili ya kutekeleza Ibada ya hijja.
Bin Asfari kutoka Sham akasema: ninashuhudia kuwa wewe ni mtoto wa nabii na Ali bin Abi Twalib ni Khalifa na wasii wa mtume Muhammadi na kwamba Ali bin Abitwalib, ndiye unaestaili uongozi kuliko Muawiya.