Maajabu ya Aliy [a.s.]
Bwana mmoja amlimjia amirul muminiina Ali bin Abi twalibi a.s na kumwambia kwamba mimi ni mjumbe nimetumwa na Muawiyah, nije nikuulize maswali ambayo yeye, aliulizwa na na Bin Asfari kutoka Sham na akashindwa kuyajibu.
Bin Asfari alimuuliza Muawiyah akisema: Ikiwa kweli wewe ni khalifa wa mtume Muhammad s.a.w nijibu maswali yangu, ukinijibu basi nitakuwa muislamu na nitalipa kodi zote zinazohitajika, Muawiaya amekosa jibu na kubaki akitahamaki hajui lakufanya, ndio maana amenituma kwako, nimlete Bin Asfar akusaili ewe Ali bin Abitwalib!
Ali a.s akauliza ni maswali gani hayo?
Akasema kwamba maswali haya ni: 1- kuna hatua ngapi baina ya haki na batili, 2-na ngapi kati ya mbingu na aridhi, 3-na ngapi kati ya mashariki na magharibi, 4-na kuhusu huu mlima, 5-nakuhusu upinde wa mvua (penamnongo), 6- na kuhusu ufuto ambao umo katika mwezi, 7- na kuhusu kitu cha kwanza kilicho ng’aa juu ya ardhi, 8- na kuhusu kitu cha kwanza kilicho tikisika katika ardhi, 9- na kuhusu chemchem inayo endewa na roho za waislamu, 10-na kuhusu chemchem inayo endewa na roho za makafiri, 11-na kuhusu jike dume, 12- na kuhusu vitu kumi ambavyo baadhi yake ni imara kuliko vyengine?
Ali bin Abi Twalib akasema niitiyeni wanangu Hasan na Husein, walipokuja, Ali bin Abi Twalib alimwambia mtu wa Sham, Swali lako ni jepesi sana kwangu,wacha wakujibu hawa wanngu, hawa ni wajukuu wa mtume Muhamad s.a.w, mchague mmoja kati yao akujibu maswali yako.
Bin Asfari alimchagua Hasan na kumuuliza maswali hayo, kwa kuwa Hasan alikuwa ni mdogo, Ibn Asfari alimbeba na kumuweka mapajani mwake.
Kisha Hasan a.s alianza kumjibu kwa kusema:
Ewe ndugu uliye tokea Shamu, 1-kati ya haki na batili kuna hatua ya vidole vinne (aliweka vidole vyake vya mkono kati ya macho na masikio yake) na kusema: Aghlabu ya uyaonayo kwa macho yako ni haki na unasikia batili nyingi kwa masikio yako, basi mtu wa Shamu, akasema: swadakta nikweli, Mungu akubariki.
2-na kati ya mbingu na aridhi kuna maombi ya walio dhulumiwa na yoyote akisema kinyume na haya huo utakuwa ni uwongo kutoka kwake, Mtu wa Shamu akasema nikweli swadakta nikweli, Mungu akubariki.
3-na kati ya mashariki na magharibi kwasiku linakukataza jua unalitazama linapo chomoza na linapo zama, na yoyote akisema kinyume na haya huo utakuwa ni uwongo kutoka kwake, akasema nikweli Mungu hakufanyie uwepesi,
4-na kuhusu hii milima ni nguzo ya mbingu na kutoka katika baadhi ya milima hii yanamiminika maji mazuri,
5-na ama upinde wa mvua (penamnongo) ni jina la shetani na huo upinde wa Mungu ni amana ili pasitokee maangamizi,
6- na ama ufuto ambao umo katika Mwezi, ulikuwa kama mwanga wa Jua Mungu akaufuta kama alivyo sema Mwenyezi Mungu {Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku, na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu tumekifafanua waziwazi.} Qur ani 17:12,
7- na kitu cha kwanza kilicho ng’aa juu ya ardhi ni jangwa la Dalsi.
8- na kitu cha kwanza kilicho tikisika humo ni mtende,
9- na chemchem inayo endewa na roho za waislamu inaitwa Salmiy.
10-na chemchem inayo endewa na roho za makafiri inaitwa Barhuuti.
11- na jike dume ni binaadamu hajijuwi ni mwanamke au mwanaume anangojea akiwa mwanaume atajiotelea na kama mwanamke ataanza kuchomoza na kukua matiti yake.
12- na vitu kumi ambavyo baadhi yake imara kuliko vyengine ni jiwe, Mungu ameliumba imara na imara kuliko jiwe ni Chuma, ambacho kinavunja jiwe na imara kuliko Chuma ni Moto, na imara kuliko Moto ni Maji, na imara kuliko maji ni Mawingu, na imara kuliko mawingu ni Upepo, na imara kuliko upepo ni Malaika, na imara kuliko malaika ni malaika mtoa roho (Izraail), na imara kuliko malaika mtoa roho ni Kifo, na imara kuliko kifo ni Amri ya Mungu mola wa viumbe wote.
Bin Asfari kutoka Sham akasema: ninashuhudia kuwa wewe ni mtoto wa nabii na Ali bin Abi Twalib ni Khalifa na wasii wa mtume Muhammadi na kwamba Ali bin Abitwalib, ndiye unaestaili uongozi kuliko Muawiya.