3 Mei 2025 - 23:21
Source: Parstoday
Msuguano wa India na Pakistan: Bidhaa za Pakistan zapigwa marufuku kuingia India

India imetangaza kuzipiga marufuku bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka au kupitia Pakistan. Mamlaka ya biashara za kigeni ya India imetangaza kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa mara moja hali inayoashiria kushadidi mvutano baina ya mataifa hayo.

Mamlaka husika imesema sababu za kuchukua hatua hiyo ni kulinda sera ya umma na maslahi ya kiusalama ya taifa hilo. India imechukua hatua hiyo wakati nchi hizo mbili zikikabiliwa na mivutano iliyochochewa zaidi na shambulio baya katika jimbo la Kashmir zinaloligombea.

Mzozo wa sasa kati ya India na Pakistan umeibuka baada ya watu waliokuwa na silaha kulifyatulia risasi kundi la watalii katika eneo la kitalii la Pahalgam, lililoko takriban kilomita 90 kutoka Srinagar, mji mkuu wa majira ya joto wa Kashmir inayodhibitiwa na India, na kuua watu wasiopungua 27.

Msuguano wa India na Pakistan: Bidhaa za Pakistan zapigwa marufuku kuingia India

Maafisa wa serikali ya India wamelitaja tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi. India inamtuhumu jirani yake wa magharibi (Pakistani) kuwa imehusika katika shambulio dhidi ya watalii huko Kashmir.

Baada ya tuukio hilo kumeshuhudiwa uruushianaji maneno na vitisho kutoka kwa pande mbili.

Jumatano iliyopita, Waziri wa Habari wa Pakistan, Attaullah Tarar alisema kwamba nchi yake ina taarifa za kuaminika za kiintelijensia kwamba India inakusudia kufanya shambulizi la kijeshi dhidi ya Pakistan ndani ya masaa 24 hadi 36 yajayo, hilo likiwa tishio la hivi karibuni zaidi la vita kati ya majirani hao wawili wenye silaha za nyuklia.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha