Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekanusha kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Iran inaomba kufikiwa kwa makubaliano, akisisitiza kuwa ni Washington ambayo imekuwa ikiomba mazungumzo mara kwa mara huku Tehran ikitaka suluhisho la kudumu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Iran itatoa jibu la haraka na la maamuzi kwa hatua yoyote ya uhasama, akisisitiza kuwa malengo yaliyoshindikana kufikiwa kwa vikwazo na vita hayawezi kupatikana kwa vita zaidi.