Mawaziri wa Michezo na Vijana wa Iran na Azerbaijan wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika diplomasia ya michezo, kubadilishana wanamichezo na makocha, pamoja na kuandaa kambi na mashindano ya pamoja.
Balozi wa Iran nchini Azerbaijan, Mojtaba Demirchilou, amesema ujenzi wa kituo cha kupakia na kupakua mizigo ya reli ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Iran na Jamhuri ya Azerbaijan, huku akitangaza kuwa mradi huo utafuatiliwa kwa karibu.
Ilham Aliyev, Rais wa Azerbaijan, ametangaza kuwa nchi yake haina mpango wa kutuma vikosi vyake kushiriki katika operesheni za kulinda amani nje ya mipaka ya nchi, ikiwemo Gaza.