Mawaziri na wawakilishi wa nchi wanachama wa D-8 wamepitisha Azimio la Baku, wakisisitiza kuimarisha ushirikiano katika usalama wa nishati, nishati jadidifu na maendeleo ya miundombinu ya pamoja ili kukabiliana na changamoto za sasa za sekta ya nishati duniani.
Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kupitia Tamko la Baku limesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha sekta za ubunifu na diplomasia ya kitamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu.