Akizungumza na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (ABNA) Jumapili, 20 Mehr 1404 (2025), Ayatullah Malakooti alisisitiza umuhimu wa kueleza Ushia kwa usahihi mbele ya upotoshaji. Alieleza kuwa kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, dunia haikuufahamu Ushia kama ilivyostahili; taarifa nyingi zilizokuwepo zilitokana na maandiko ya Ahlus-Sunnah yaliyo na taarifa zisizokamilika au kwa makusudi kutoeleza Ushia kwa usahihi, na hivyo Ushia / Mashia walichukuliwa kama kundi dogo au la upande mmoja.