Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara wa Iran amesema Tehran imejipanga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi wanachama wa Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia kupitia utekelezaji wa makubaliano ya biashara huria, maendeleo ya njia za usafirishaji na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kibenki.
Kwa mujibu wa Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Mohammad Atabak, maazimio ya kimkakati yaliyopitishwa katika kikao cha pili cha Baraza la Pamoja la Serikali za Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia yanatarajiwa kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi na kuongeza kiwango cha biashara kati ya Iran na nchi wanachama wa umoja huo.