Kwa mujibu wa Madrasatu Ahlul-Bayt (a.s.), tukio la Ghadir Khum halikuwa la kutangaza mapenzi na heshima kwa Imam Ali (a.s.) pekee, bali lilikuwa tangazo la Mwenyezi Mungu kuhusu Wilayah na uongozi wake baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), jambo linalodhihirisha umuhimu wa kuwepo kwa kiongozi wa Umma baada ya Mtume (saww).
Sikukuu ya Ghadir, ambayo ni miongoni mwa sikukuu kubwa zaidi kwa Waislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna Ashari, ambapo huadhimisha ndani yake kutangazwa kwa wilayat ya Imam Ali ibn Abi Talib(as). Katika siku hii, Waumini huhimizwa kufanya amali mbalimbali za ibada na kheri kama vile kuswali, kusoma dua, kutoa sadaka na kuwalisha wengine, huku wakitumia fursa hiyo kuimarisha maarifa ya dini, kuhuisha ahadi yao katika kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na kuimarisha mshikamano wa kijamii na kiroho.