Mkoa wa Hadhramaut, eneo kubwa zaidi na lenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Yemen, kwa sasa umegeuka kuwa kitovu cha ushindani kati ya Saudi Arabia na Falme za Kiarabu. Licha ya vita vilivyoendelea kwa zaidi ya muongo mmoja, Hadhramaut kwa kiasi kikubwa imeepuka mapigano ya moja kwa moja kati ya serikali ya Yemen iliyojiuzulu na serikali inayoungwa mkono na Harakati ya Ansarullah; hata hivyo, mkoa huu haujaepuka athari za vita na mashindano ya ushawishi wa ndani na kikanda.