Katika taarifa ya Hizbullah na Harakati ya Amal ilisemwa: 'Enyi wafanyakazi na wazalishaji wa Lebanon, tumekuwa wavumilivu kwa muda mrefu juu ya changamoto zinazolikumba taifa letu, na sasa umefika wakati wa kuonyesha msimamo wetu wa kitaifa kwa pamoja.'
Wakaongeza: 'Tuna miadi ya kusimama kwa pamoja kama taifa, kuonyesha kupinga kwetu njia ya kujisalimisha na kutii bila masharti, na kulinda nguvu na uhuru wa Lebanon'.