Nadhami Ardakani ametaja kaulimbiu ya “Mkutano Mkuu wa Nne wa Masadat” kuwa:
"Masadat ni Wabeba Bendera wa Mapambano dhidi ya Utawala wa Kizayuni na Watunzi wa Historia ya Baadaye",
na akasema: Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, bendera ya kupambana na Uzayuni ilipeperushwa kwa mara ya kwanza na Imam Khomeini (r.a), kisha ikakabidhiwa kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ambaye mwenyewe ni katika Masadat, na baadaye ikaendelezwa na watu kama Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Sayyid Badruddin Houthi na Ayatollah Sistani.