Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Hujjatul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, amesema ataelekeza uwezo wake wote katika kutekeleza majukumu aliyopewa baada ya kuteuliwa tena kuongoza mhimili huo.
Mkuu wa Mahakama ya Iran amesema njama za maadui za kuisambaratisha Iran zimeshindwa, akisisitiza kuwa uimara wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na mshikamano wa wananchi umezuia machafuko na kuimarisha nafasi ya Iran duniani.