Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hujjatul-Islam Gholam Hossein Mohseni Ejei, amesema atafanya kila juhudi kuhakikisha anatekeleza kwa ufanisi na uaminifu majukumu aliyokabidhiwa kufuatia kuteuliwa tena kuongoza mhimili huo.
Katika ujumbe alioutuma kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei, akijibu uamuzi wa kumteua tena, Mohseni Ejei alieleza shukrani zake kwa imani aliyopewa na kuahidi kutumia uwezo wake wote katika kuhudumia mfumo wa haki na wananchi.
Aidha, amesema kuwa maelekezo na wasia wa Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na miongozo iliyotolewa na Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei katika ujumbe wake wa maadhimisho ya Wiki ya Mahakama ya mwaka huu, yatakuwa dira na msingi wa kazi zake pamoja na watumishi wote wa mhimili wa mahakama.
Your Comment