Msemaji wa Kamati ya Sherehe za Umma za Ghadir Khumm alisema kuwa sherehe hii imeenea kwa zaidi ya miji 500 nchini Iran na katika nchi 20 duniani. Mwaka huu, tunatarajia kupika zaidi ya sufuria 30,000 za chakula cha moto, kushirikishwa kwa zaidi ya watumishi 100,000 mjini Tehran, kuwepo kwa mabaraza (Mawa'qib) ya umma 2,400 na kuanzishwa kwa mbuga za michezo kwa watoto milioni moja; yote haya kwa upendo wa Wilaya ya Amirul Momineen (a.s).