Hafla ya kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad Mustafa (saw) imefanyika katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, ikishirikisha wanafunzi, walimu na waumini kutoka jamii ya Waislamu wa Shia na Sunni. Hotuba katika hafla hiyo imeangazia fadhila, tabia njema na mwenendo wa Mtume (saw), pamoja na upendo wake kwa watoto na umuhimu wa malezi bora ya kizazi kijacho.
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, amesisitiza umuhimu wa umoja wa Mashia, Waislamu na watu wa dini mbalimbali, pamoja na uzalendo na kuheshimu viongozi wanaolitumikia taifa na jamii kwa uadilifu.