21 Julai 2026 - 08:25
Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, amesisitiza umuhimu wa umoja wa Mashia, Waislamu na watu wa dini mbalimbali, pamoja na uzalendo na kuheshimu viongozi wanaolitumikia taifa na jamii kwa uadilifu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-  Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, jana alihudhuria na kuongoza majlisi ya kumbukumbu ya Sayyid Ali Khamenei, iliyofanyika katika Husseiniyat Zahra (as), Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji.

Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei

Maulana Sheikh Hemed Jalala alikuwa katika ziara yake Wilaya ya Rufiji alipohudhuria majlisi hiyo, ambapo katika mawaidha yake alieleza kuwa kuna mafunzo matano muhimu yanayoweza kupatikana kutokana na mazishi ya Sayyid Ali Khamenei.
 
Akitaja mafunzo hayo, Maulana alisema la kwanza ni umuhimu wa umoja wa Mashia; la pili ni umoja wa Waislamu bila kujali tofauti za madhehebu; la tatu ni umoja wa watu wa dini mbalimbali katika kuthamini utu na mshikamano.

Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei

Aliongeza kuwa fundisho la nne ni uzalendo na kuipenda nchi, huku la tano likiwa ni umuhimu wa kuwaheshimu na kuwapenda viongozi wanaolitumikia taifa na jamii kwa uadilifu.

Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei

Maulana Sheikh Hemed Jalala aliwataka waumini kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika maisha yao ya kila siku, akisisitiza kuwa utekelezaji wake utasaidia kuendelea kujenga jamii yenye umoja, amani, uzalendo na maadili mema.

Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha