Muhimu
-
Maulana Sheikh Hemed Jalala Atoa Mafunzo Matano Muhimu Kutokana na Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei
Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, amesisitiza umuhimu wa umoja wa Mashia, Waislamu na watu wa dini mbalimbali, pamoja na uzalendo na kuheshimu viongozi wanaolitumikia taifa na jamii kwa uadilifu.
-
Zaidi ya Raia 30 Wauawa Kufuatia Mashambulizi Kusini mwa Iran, Serikali Yalaani Vikali
Serikali ya Iran imelaani vikali mashambulizi yaliyolenga maeneo ya kusini mwa nchi, yakisababisha vifo vya zaidi ya raia 30, huku ikithibitisha kuwa huduma muhimu na misaada kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika vinaendelea bila kusitishwa.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Elimu ya Akili Bandia na Usalama wa Mtandao ni Muhimu Shuleni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesisitiza umuhimu wa kufundisha akili bandia (AI) na usalama wa mtandao katika shule kwa mtazamo wa vitendo na unaojenga ujuzi, akieleza kuwa teknolojia za kisasa zina nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto za kisasa.
-
Rais Pezeshkian: Umoja na Mshikamano Ndiyo Rasilimali Kubwa Zaidi ya Iran
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa umoja na mshikamano wa kitaifa ndio nguzo muhimu zaidi ya nchi, akibainisha kuwa mshikamano wa wananchi umefutilia mbali mipango ya maadui ya kuleta machafuko nchini humo.
-
Meloni Aishukuru Qatar na Pakistan kwa Kufanikisha Makubaliano ya Marekani na Iran
Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, ameishukuru Qatar, Pakistan na wapatanishi wengine kwa mchango wao katika kufanikisha makubaliano kati ya Marekani na Iran, akisema juhudi zao zimefungua ukurasa mpya wa diplomasia na amani katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
Rais Pezeshkian: Juhudi za Pakistan Zitabaki Kwenye Kumbukumbu ya Wairan Milele
Rais wa Iran ameipongeza Pakistan kwa juhudi zake za dhati katika upatanishi uliochangia kufikiwa kwa makubaliano ya awali ya kumaliza vita, huku Tehran na Islamabad zikiahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kwa ajili ya amani na maendeleo ya kikanda.
-
Rais wa Iran Aishukuru Qatar kwa Jukumu Lake la Kupunguza Mvutano na Kuendeleza Diplomasia
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameipongeza Qatar kwa mchango wake katika kupunguza mvutano wa kikanda na kuwezesha juhudi za kidiplomasia zilizopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita.
-
Jarida la Foreign Affairs: "Uwezo wa Marekani Hautoshi Tena Kutimiza Malengo Yake ya Kimataifa"
Uchambuzi wa jarida la Foreign Affairs unasema kuwa kuongezeka kwa vitisho katika Mlango wa Hormuz na maendeleo ya teknolojia za kijeshi kumeonyesha pengo kati ya matarajio ya kimataifa ya Marekani na uwezo wake halisi wa kudhibiti usalama wa bahari duniani.
-
UMOJA WA MATAIFA: Nusu ya Wakazi wa Afghanistan Wanahitaji Msaada wa Kibinadamu
Ofisi ya Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa mwaka 2026 takribani watu milioni 22 — sawa na asilimia 45 ya watu wa Afghanistan — watahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu; huku idadi ya watu wenye uhaba mkali wa chakula ikifikia milioni 17.4 na milioni 5.2 wakiwa katika hatari ya njaa kali.
-
Nafasi Muhimu ya Nahjul-Balagha katika Elimu ya Bara Hindi:
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) na Kituo cha Fikra za Kiislamu Waandaa Webina ya Kimataifa Kuhusu Nafasi Muhimu ya Nahjul-Balagha katika Elimu
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kushirikiana na Kituo cha Fikra za Kiislamu wameandaa webina ya kimataifa iliyopewa jina: “Hadhi ya Nahj al-Balagha katika Bara la Hindi na Nafasi Yake katika Elimu.” Tukio hili limefanyika Jumamosi, tarehe 15 Novemba 2025.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala
Ayatollah Khamenei katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 32 wa Kitaifa wa Sala alielezea mambo muhimu yanayohusu mkutano huu pamoja na sifa za sala.