Italia
-
Italia na Hispania Zimetuma Manowari za Kivita kwa ajili ya Kulinda Msafara wa Meli za Sumuud
Kufuatia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya msafara wa kimataifa wa Sumuud (Jina la Msafara), ambao unalenga kupeleka misaada ya kibinadamu kwa Gaza na ulikuwa ukisafiri katika maji ya kimataifa, Italia na Uhispania zimetuma meli zao za kivita ili kuhakikisha usalama wa msafara huo. Hatua hii imechukuliwa baada ya kulaaniwa kwa kiwango kikubwa kwa mashambulizi hayo dhidi ya meli zisizo za kijeshi, ambayo yamechukuliwa kuwa ni uvunjaji wa sheria za kimataifa.
-
Jeshi la Italia Lakamata Meli ya Mizigo ya Silaha Inayodaiwa Kutoka Saudi Arabia Kwenda Israel
Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, silaha hizo zinadaiwa kuwa sehemu ya mpango mpana wa usafirishaji wa vifaa vya kijeshi kuelekea Israel, wakati huu ambapo mapigano na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza yanaendelea.
-
Raundi mpya ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani itafanyika Ijumaa hii Mjini Rome, Italia
Raundi ya tano ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa mjini Rome, Italia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza kuwa nchi yake imekubali pendekezo la Oman kwa ajili ya kikao hiki. Aidha, alisisitiza kuwa ujumbe wa Iran katika mazungumzo haya umejikita katika kulinda haki za taifa hilo na kuhakikisha kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran.