Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kazem Gharibabadi, amesema kuwa Iran na Oman ndizo pekee zenye haki ya mamlaka juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz, akisisitiza kuwa hakuna nchi nyingine inayopaswa kuingilia usimamizi wa njia hiyo muhimu ya baharini.
Balozi wa Iran nchini Iraq, Mohammad Kazem Al-Sadeq, amekutana na Patriarki (Baba-Kiongozi) mpya wa Kanisa la Kaldania, Mar Paulus III Nona, jijini Baghdad ambapo pande hizo zimesisitiza umuhimu wa kuimarisha maelewano ya kijamii, kuishi kwa amani kati ya dini mbalimbali na kuendeleza ushirikiano wa kikanda.