Ayatollah Khamenei, katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 59 wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya, amesisitiza kuwa sababu kuu ya msukosuko na wasiwasi wa madhalimu wafisadi si suala la nyuklia, bali ni kuinuliwa kwa bendera ya kupinga mfumo usio wa haki na utawala wa mabavu wa mfumo wa ubeberu duniani, pamoja na mwelekeo wa Iran ya Kiislamu kuelekea kujenga mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s), akiwa mbele ya wakurugenzi na wafanyakazi wa Mahakama ya Mkoa wa Gilan, amesema kuwa utekelezaji sahihi wa haki na usawa katika taasisi zote za serikali unaweza kuongeza ufanisi wa Jamhuri ya Kiislamu na kuthibitisha madai yake ya msingi kuhusu haki katika utawala.