Kinachoendelea katika shambulizi la Israel dhidi ya Beirut ni kama ifuatavyo:
Mashambulizi ya Israel Kusini mwa Beirut yanaonyesha kuendelea kwa mivutano ya kikanda, huku ukiwepo msisitizo kuwa Muqawama - Upinzani- wa Lebanon (Hezbollah) unaona una uhalali wa kukabiliana na jaribio lolote la adui Israel katika kubadilisha mlingano wa usalama katika nchi ya Lebanon.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeua mashahidi 6 Wapalestina na kuwajeruhi watu 5 wengine, baada ya kulipua kwa mizinga kituo cha hifadhi kilichopo mashariki mwa Jiji la Gaza, wakati wa hafla ya harusi.