Kuchangia

  • Ayatollah Ramezani: Wanawake Wana Nafasi Kuu katika Ujenzi wa Ustaarabu wa Kiislamu na Mabadiliko ya Kijamii

    Ayatollah Ramezani: Wanawake Wana Nafasi Kuu katika Ujenzi wa Ustaarabu wa Kiislamu na Mabadiliko ya Kijamii

    Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s.), akisisitiza nafasi ya mwanamke katika Qur’ani Tukufu na mafundisho ya Kiislamu, amebainisha umuhimu wa wanawake katika malezi ya kizazi, kuimarisha misingi ya familia na kuleta mabadiliko ya kijamii. Amesema kuwa mfano wa mwanamke Mwislamu ni mwanamke mwenye imani, elimu, busara, uchamungu na maadili ya Mwenyezi Mungu; na kwamba Hazrat Fatima Zahra (s.a.) ndiye mfano bora wa kuigwa kwa wanawake katika kutekeleza majukumu yao katika jamii na kuchangia ujenzi wa ustaarabu wa Kiislamu.