Jumuiya ya Al-Wefaq: Mawasiliano ya Mfalme wa Bahrain na Rais wa utawala wa Kizayuni yanakwenda kinyume na maslahi ya taifa
Jumuiya ya Al-Wefaq imelaani vikali mawasiliano ya simu kati ya Mfalme wa Bahrain na Rais wa utawala wa Kizayuni, ikieleza kuwa hatua hiyo ni kujitenga na msimamo wa pamoja wa kitaifa na wa wananchi wa Bahrain.
Katika taarifa yake, Al-Wefaq imesema kuwa kitendo hicho kinaonyesha utegemezi wa serikali ya Bahrain kwa ajenda za Marekani na utawala wa Kizayuni, na kwamba hakilingani na matakwa ya wananchi wala maslahi ya taifa.
Aidha, jumuiya hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo ni kinyume na maslahi na usalama wa Bahrain, ulimwengu wa Kiarabu na Umma wa Kiislamu, ikisisitiza kuwa kuimarisha uhusiano na utawala wa Kizayuni hakutaleta amani wala utulivu katika eneo, bali kutaongeza migogoro na kuhatarisha usalama wa kikanda.