Si lazima kila mara jambo litokee kutoka mbinguni na kila kitu kibadilike kwa usiku mmoja. Wakati mwingine msaada wa Mwenyezi Mungu huwa katika mkono uleule ambao, licha ya uchovu, huinuka tena. Huwa katika mpiganaji ambaye, licha ya hofu, husonga mbele. Huwa katika mama ambaye moyo wake hutetemeka, lakini anamsindikiza mwanawe kwenda kutetea haki.
Msaada wa Mwenyezi Mungu wakati mwingine hujidhihirisha katika uamuzi sahihi, moyo imara na umoja wa watu.
Maelfu ya waumini wa Ahlul-Bayt (as) jijini Dar es Salaam wamefanya Masira ya A'shura katika Wilaya ya Temeke kwa lengo la kuhuisha ujumbe wa Imam Hussein (as), kulaani mauaji ya Karbala na kusisitiza kusimama upande wa haki, uadilifu na kupinga dhulma.