Mkurugenzi Mkuu wa Tablighi za Kiislamu mkoa wa Fars ameeleza kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya Kimungu ya kujenga upya roho na kurekebisha mtindo wa maisha. Amesema kuwa Mwenyezi Mungu ameumba mfumo wa uwepo wa mwanadamu kwa namna ambayo katika kipindi fulani cha mwaka huhitaji mabadiliko katika namna ya kuishi na kula; mabadiliko ambayo hupelekea kuinuka kwa roho na kuimarika kwa irada.
Ramadhani ni uwanja wa mazoezi ya ibada na kujijenga nafsi, na kwa tafsiri nyingine ni hundi nyeupe yenye saini ya Kimungu kwa ajili ya msamaha na kuangazwa kwa nyoyo.