Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kutoka Fars, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Baqir Woldan, alasiri ya Jumapili akiwa katika mkusanyiko wa wafanyakazi wa Jeshi la Nchi Kavu la Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alieleza kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya Kimungu ya kujenga upya roho na kurekebisha mtindo wa maisha. Alisema Mwenyezi Mungu ameumba mfumo wa uwepo wa mwanadamu kwa namna ambayo katika kipindi fulani cha mwaka huhitaji mabadiliko katika namna ya kuishi na kula; mabadiliko ambayo hupelekea kuinuka kwa roho na kuimarika kwa irada. Ramadhani ni uwanja wa mazoezi ya ibada na kujijenga nafsi, na kwa tafsiri nyingine ni hundi nyeupe yenye saini ya Kimungu kwa ajili ya msamaha na kuangazwa kwa nyoyo.
Akiashiria fadhila za mwezi huu, aliongeza kuwa katika Ramadhani usingizi wa muumini ni ibada na pumzi yake ni thawabu, na kusoma kila aya ya Qur’ani Tukufu kuna malipo makubwa. Milango ya Jahannam hufungwa na milango ya Pepo hufunguliwa ili nyoyo za waumini zipate utulivu na kuokoka na moto wa ndani pamoja na wasiwasi wa kishetani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Tablighi za Kiislamu mkoa wa Fars, akisisitiza nafasi ya Qur’ani katika kuleta utulivu wa nafsi, alisema: Qur’ani ni kitabu cha utulivu na ramani ya njia ya saada ya mwanadamu; kama ilivyokuja katika aya tukufu: “Alaa bidhikriLlah tatma’innul quluub” - hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia - na kushikamana na Qur’ani humlinda mwanadamu katika misukosuko ya fitna za zama za mwisho.
Aidha, akikumbusha Hadithi ya Thaqalayn, alisisitiza kuwa Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad (s.a.w.w), aliacha amana mbili zenye thamani kubwa - Qur’ani na Ahlul-Bayt (as) - kwa ajili ya uongofu wa umma, na akabainisha kuwa kushikamana na viwili hivyo ni sharti la kuokoka na upotovu. Kwa sababu hiyo, uhusiano kati ya Qur’ani na Imam Mahdi (a.t.f.s) ni uhusiano usiotenganika.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Woldan aliendelea kwa kuashiria mpango wa “Kuishi na Aya” na kusema: Katika kipindi hiki cha televisheni, kila siku huchaguliwa aya moja kutoka juzuu ya siku hiyo na kufasiriwa ili kuandaa mazingira ya watu kuzoea zaidi mafundisho yenye nuru ya Qur’ani.
Ameongeza kuwa katika siku ya nne ya Mwezi wa Ramadhani, aya ya 173 ya Suratul Aal-Imran ndiyo mhimili wa mahafali ya Qur’ani, na kauli “Hasbunallahu wa ni‘mal Wakiil” ni kaulimbiu ya utegemezi wa moyoni kwa waumini mbele ya magumu na changamoto. Tunapaswa kwa nuru ya Kimungu kusafisha nyoyo zetu kutokana na vumbi la maisha ya kila siku na kujiandaa kwa ajili ya Laylatul-Qadr, ili kumbukumbu ya Imam Mahdi (a.f.) iwe pambo la vikao na nyoyo zetu.
Your Comment