13 Juni 2026 - 16:52
Serikali ya Iran Yatangaza Mali Zilizoachwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (r.a)

Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uchunguzi wa mali za Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) umebaini kuwa aliacha mali chache sana, jambo linalotajwa kuakisi maisha yake ya ucha-Mungu na kujiepusha na anasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza matokeo ya uhakiki wa mali zilizoachwa na Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (r.a.), ikisema kuwa mali yake binafsi ilikuwa ndogo sana.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mali zote alizomiliki zimeorodheshwa na zinajumuisha gari dogo la kubebea mizigo, huku ikielezwa kuwa hakuwa na nyumba za kifahari, kampuni, akaunti za benki zenye utajiri mkubwa wala mali zilizofichwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Ayatollah Khamenei (r.a.) alitumikia kwa takribani miaka 47 kama Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliwahi pia kuwa Waziri wa Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kwa karibu miaka 40 alikuwa Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo.

Aidha, imeelezwa kuwa licha ya kuwa alikuwa Marjaa wa Kidini aliyefuatwa na mamilioni ya waumini duniani, aliendelea kuishi maisha ya kawaida na ya kujisitiri hadi mwisho wa maisha yake.

Serikali ya Iran imeeleza kuwa hali hiyo inaonesha mfano wa uadilifu, kujiepusha na matumizi ya mali ya umma na kujitolea kuitumikia jamii kwa uaminifu.

Taarifa hiyo pia imeambatana na picha ambayo ilipigwa muda mfupi kabla ya kuuawa Shahidi kwa Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Tanbihi: Taarifa hii inatokana na tamko lililotolewa na Serikali ya Iran na si vinginevyo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha