Kamanda wa Makao Makuu ya Pamoja ya Ulinzi wa Anga nchini Iran, Brigedia Jenerali Alireza Elhami, amesema kusasisha vifaa, uwezo na mitaala ya mafunzo ni jambo la lazima ili kukabiliana na mabadiliko ya vitisho vya anga na maendeleo ya teknolojia za kijeshi.
Timu ya taifa ya wanawake ya volleyball ya Iran imeendelea kuonesha ubabe wake katika ukanda wa Asia ya Kati baada ya kutwaa ubingwa wa Mashindano ya CAVA 2026 kwa kuifunga Kazakhstan mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika mjini Kathmandu, Nepal.
Hujjatul Islam wal Muslimin Muhammad Saeed Waezi amesema kuwa kuimarisha umoja na mashauriano kati ya wanazuoni na wasomi wa Kiislamu ni jambo muhimu katika kukabiliana na changamoto za sasa na kufikia malengo makubwa ya ustaarabu mpya wa Kiislamu.