Majina haya ya heshima (Lakabu) hayakuwa tu kwa lengo la kuitana (ili mradi kuitana, pasina kuwepo kigezo chochote cha msingi), bali yalibeba taarifa za kiroho, madhumuni ya uongozi wa ki_Mungu, na mafunzo kwa Waislamu wote. Kujifunza kuhusu laqabu za Imamu Ridha (a.s) ni kujifunza kuhusu maisha na tabia bora za Kiislamu.
Ukufungua kurasa za Historia ya Maisha yake safi ya Imam Ali bin Abi Talb (a.s), utamkuta kwamba yeye ni wa mwanzo katika kila kitu, kisha wengine wanafuata nyuma yake katika kitu hicho.