Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-; Vitabu vingi vya historia ya Kiislamu na Hadithi za Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) vinabainisha wazi kuhusiana na suala la kutangulia kwa Imam Ali (a.s) katika Uislamu kwa mambo mengi (kwa maana sio kwa jambo moja au mawili, bali ni kwa mambo mengi), na miongoni mwa mambo ya fahari na fadhila kwa Imam Ali (a.s) ni kule kutangulia kwake katika Uislamu wenyewe. Kumkubali na kumuamini Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) tangu siku ya kwanza ulipoteremka Wahyi kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Aidha, ni pamoja na kuswali nyuma ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kusimama pamoja naye katika raha na shida.
Na suala hili la ubora wa kutangulia katika kitu au jambo, lipo (na lina msingi) ndani ya Qur’an Tukufu, kwa maana kwamba kutangulia katika Uislamu ni ubora na fadhila kwa waliotangulia katika Uislamu, na hilo ni kwa mujibu wa kauli Mwenyezi Mungu (s.w.t) aliposema:
وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنْصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُمْ بِإِحْسَانٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
“Na waliotangulia wa kwanza katika wahajiri na Ansari. Na wale waliowa[1]fuata kwa wema, Mwenyezi Mungu yuko radhi nao na wao wako radhi Naye; na amewaandalia Bustani ambazo hupita mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.” (Surat Al-Tawba: Aya ya 100).
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni wa mwanzo kati ya wale waliom[1]wamini Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w), kama vile alivyokuwa wa awali na aliyewatangulia watu wengine wote katika kila jambo la kheri.
Tunapopekua na kuperuzi kurasa mbalimbali za Historia safi za Imam Ali bin Abi Talib (a.s), tuna[1]kuta kwamba yeye ni wa mwanzo katika kila kitu.
Mfano hai: Imam Ali bin Abi Talib (a.s) ni mtu wa mwanzo kabisa kuukubali Uislamu, na ni wa mwanzo kuswali pamoja na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w). Wkati wengine wakiwa kwenye kuabudia Masanam, yeye yuko katika swala na Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) wakimuabudu Mwenyezi Mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki.
Imam Ali (a.s) wa Kwanza Kuitwa kwa Lakabu ya Amirul-Muuminina (Kiongozi wa Waumini)
Kama tulivyoashiria, ukufungua kurasa za Historia ya Maisha yake safi ya Imam Ali bin Abi Talb (a.s), utamkuta kwamba yeye ni wa mwanzo katika kila kitu, kisha wengine wanafuata nyuma yake katika kitu hicho.
ifuatayo ni sehemu ya mifano zaidi juu ya ukweli huu:
Imam Ali (a.s) ni wa mwanzo katika Uislamu, na ni mtu wa kwanza kupewa Lakabu ya Amirul-Muuminina (Kiongozi wa Waumini), na aliyempa Lakabu hiyo ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) kupitia Mjumbe wake Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) pia ni mtu wa kwanza aliyekusanya Qur’an Tukufu (baada ya kufariki kwa Bwana Mtume s.a.w.w), na akaweka misingi ya elimu zake.
Imam Ali (a.s) Ni Mwanafunzi wa kwanza wa Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) ni mtu wa kwanza aliyembai (alyempa Bai’a au kiapo cha utii) Mtukufu Mtume Muhammad(s.a.w.w), na akatangaza kumnusuru.
Imam Ali (a.s) ni Mwandishi wa kwanza wa Wahyi uliokuwa ukishuka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) ni mtu wa kwanza kupewa uongozi na usimamizi wa mambo juu ya Waislamu.
Imam Ali (a.s) ni mtu wa kwanza kuitoa muhanga nafsi yake kwa ajili ya kuokoa uhai wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) mtu wa kwanza kupigana vita (Jihadi) katika Njia ya Mwenyezi Mungu.
Imam Ali (a.s) ni mtu wa kwanza kubeba Bendera ya Uislamu mbele ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) ni wa kwanza kufikisha Ujumbe wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) ni kadhi wa kwanza katika Dini Tukufu Uislamu (Baada ya Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w.w).
Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza kusema akiwambia watu wote "niulizeni kabla hamjanikosa". Hakuna mwingine aliyewahi kusema kauli hii, kwa sababu yeye ndiye mlango wa elimu yote ya Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w).Mtume (s.a.w.w) abasema: "Mimi ni Mji wa Elimu na Ali ni Mlango wake".
Imam Ali (a.s) ndiye Mwislamu wa kwanza ambaye Mtume Muhammad (s.a.w.w) hakumwamrisha yeyote kuwa juu yake.
Imam Ali (a.s) ni Khalifa wa kwanza wa ukoo wa Bani Hashim.
Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza kuweka Katiba iliyokamilika ya Dola na Serikali ya Kiislamu.
Imam Ali (a.s) ni mtu wa kwanza kuandika vitabu katika Uislamu.
Imam Ali (a.s) ndiye mtua kwanza aliyeweka Elimu ya Nahawu.
Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza aliyeasisi Elimu ya Theiolojia katika Uislamu.
Imam Ali (a.s) ndiye mtu wa kwanza kuzaliwa Msikitini (ndani ya Al-Kaaba Tukufu) na kufa kifo cha Kishahidi baada ya kushambuliwa na muovu Ibn Muljim (Laana iwe juu yake) alipompiga upanga wenye sumu kali kichwani mwake akiwa amesujudu Msikitini (Ndani ya Masjid Al-Kufa, akiswali Swala ya Al-Fajiri).
Na mengine mengi matukufu na yaliyo bora na yenye fadhila kemkem ambayo utamkuta Imam Ali (a.s ) akiwatangulia watu wote kuyafanya.
Your Comment