Sheikh Zakzaky amesema: “Kama maridhiano na madhalimu yangekuwa sahihi, basi Imam Hussein (a.s) angekubaliana na Yazid.” Sheikh Ibrahim Zakzaky, katika mkutano na kundi la wanafunzi wa vyuo vya kidini kutoka nchi kadhaa za Kiislamu, alisisitiza wajibu wa kielimu na kijamii wa wanafunzi wa dini, akiwahimiza kujifunza kwa undani elimu za Kiislamu, kuielimisha jamii, na kulinda uhuru wa fikra. Aidha, alitoa onyo kali kuhusu juhudi za kuhalalisha au kuzoesha maridhiano na madhalimu.
“Na (Kumbukeni) Ibrahim alipojaribiwa na Mola wake kwa matamko, naye akayatimiza. Akasema: Hakika mimi nitakufanya kuwa Imam wa watu. Ibrahim akasema: Je,na Kizazi changu (pia)?.(Ndiyo, lakini) ahadi yangu haiwafikii Madhalimu.”