Ujumbe wa kidiplomasia wa Oman unatarajiwa kuwasili Tehran leo kwa ajili ya kufanya mashauriano kuhusu taratibu za kusimamia usafiri wa majini katika Mlango wa Hormuz. Ziara hiyo ni sehemu ya mashauriano yanayoendelea kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Usultani wa Oman. Mashauriano hayo yanalenga kufikia taratibu zinazofaa za kusimamia na kuratibu mwenendo wa usafiri wa majini katika Mlango wa Hormuz.