Raj‘a, yaani kurejea kwa waumini waliokuwa wakamilifu kabisa na makafiri waliokuwa wabaya kabisa duniani katika kipindi cha kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.s), ni ngazi miongoni mwa ngazi za Siku ya Kiyama, na imo katika njia ya ukamilifu wa mwanadamu.
kwa Hakika Amirul-Mu'minin Ali (a.s) hakuwa anarudi kutoka vitani mpaka apate ushindi kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Na ni fadhila iliyo kubwa kiasi gani kuwa Malaika Jibril (as) anapigana upande wa kulia wake, na Mikail (as) upande wa kushoto wake.