Ayatollah Sayyid Mojtaba Husseini Khamenei, katika mkutano wake na Meja Jenerali Mohsen Rezaei, aliitaja Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na sekretarieti yake kuwa “makutano ya mikakati na mipango” ya masuala ya nchi.
Kijana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 32, Shadi Ahmad Ibrahim Ajarmeh, ameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel karibu na makutano ya Nabi Yunus, kaskazini mwa Al-Khalil, katika Ukingo wa Magharibi. Baada ya tukio hilo, wanajeshi wa Israel walichukua mwili wake. Wakati huohuo, vijana wawili wa Kipalestina walijeruhiwa wakati wa uvamizi wa wanajeshi wa Israel katika mji wa Ariha.