Matokeo ya uchaguzi wa karibuni nchini Canada yamezua ghadhabu miongoni mwa wafuasi wa utawala wa Kizayuni, hasa baada ya ushindi wa Mark Carney, mwanasiasa ambaye anajulikana kwa msimamo wake wa kihafidhina zaidi kuhusu suala la Palestina.
Mabadiliko haya katika mwelekeo wa siasa za Canada yamewafanya baadhi ya wafuasi mashuhuri wa Kizayuni kuonesha hali ya kukata tamaa, huku wakitoa ukosoaji mkali dhidi ya mazingira mapya ya kisiasa yanayoweza kuathiri uhusiano wa karibu wa Canada na Israel.Hofu kuu ya makundi hayo ni kwamba sera mpya zinaweza kupunguza uungaji mkono wa wazi kwa Israel, na kufungua nafasi kwa mijadala mikali zaidi kuhusu haki za Wapalestina katika siasa za ndani na nje ya Canada.